RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI YAKE ITAILINDA MUUNGANO KWA NAMNA YOYOTE.9


Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Mh  John  Joseph  Magufuli  amesema kuwa serikali  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania itaulinda Muungano kwa  namna  yeyote  pamoja na kuwadhibiti wale wote watakaojaribu  kuvunja  Muungano  wa  Tanganyika  na  Zanzibar.

Image result for magufuli

Tamko  hilo  amelitoa leo wakati akihutubia kwenye  sherehe ya  maadhimisho ya miaka 54 ya  Muungano  wa Tanganyika na  Zanzibar  katika  viwanja vya  Jamhuri jijini  Dodoma.

Mh Rais amesema kuwa kamwe  serikali  haitamwonea aibu , huruma  wala kumruhusu  mtu yeyote kuvuruga amani na kuvunja Muungano  wa  Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania.

Aidha  Mh Rais  wakati  akihutubia  katika  sherehe hiyo  ameeleza  baadhi ya Manufaa ya Muungano wa Jamhuri  ya  muungano  wa   Tanzaania  katika  kipindi  cha  miaka 54 tangu 1964 hadi  2018 ambapo amesema kuwa kama atatokea mtu yeyote au kundi au chama chochote  kujaribu kuvunja Muungano hawataonewa huruma iwe wa hapa nchini au nje kwani amani ni msingi wa maendeleo.

 Hali kadhalika  Katika  kipindi  cha  miaka 54  baadhi  ya  huduma  za  jamii zilizoimarishwa katika  Jamhuri ya Muungano  wa  Tanzania katika Nyanja za  kiuchumi  kisiasa  na  kijamii ni pamoja na miundombinu ya umeme ,usafiri wa  nchi kavu na majini,upatikanaji wa huduma za jamii kama elimu, afya ,na baadhi ya huduma za elimu na afya kuongezeka mara dufu.

Hata  hivyo   Kauli  mbiu  ya  sherehe  ya  Muungano   wa  Tanzania   inasema   “ Miaka  54  ya Muungano wetu  ni  mfano  wa  kuigwa  duniani tuuenzi, tuulinde , tuuimarishe  na  kuudumisha  kwa maendeleo  ya  taifa  letu” . 

RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI YAKE ITAILINDA MUUNGANO KWA NAMNA YOYOTE.9 RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI YAKE ITAILINDA MUUNGANO KWA NAMNA YOYOTE.9 Reviewed by safina radio on April 26, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.