MADAKTARI NCHINI DRC WAENDELEA NA MGOMO
Madaktari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea na
mgomo wao walioanza siku ya jana kutokana na wito uliotolewa na chama chao kikuu.
Madaktari nchini DR Congo wanaomba serikali kuboresha mishahara
yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu
madai yao.
Aidha wanadai kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za
ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja
waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016
na ambao wamefanya kazi tangu wakati huo bila malipo.
Wagonjwa wameomba madaktari kusitisha mgomo huo wakisema kuwa
unawaathiri pakubwa, huku wakiomba serikali kutafutia ufumbuzi madai ya
madaktari.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, serikali imetoa mapendekezo kwa
madaktari wanaogoma na tayari imejibu madai ya madaktari hao, huku ikisema kazi
kubwa kwa sasa iko upande wa chama kikuu cha madaktari, ambacho hakikuwasilisha
mapendekzo hayo kwa wanachama wake.
MADAKTARI NCHINI DRC WAENDELEA NA MGOMO
Reviewed by safina radio
on
April 24, 2018
Rating:
No comments