SERIKALI IMESEMA KUWA BADO KUNA UWEPO WA VIASHIRIA VYA HATARI KATIKA MAZIMGIRA.
Serikali imesema kuwa licha ya juhudi mbali mbali
zinazoendelea kukabiliana na uharibifu wa mazingira na tabia nchi bado hali
inaonesha kuwepo kwa viashiria vya hatari hivyo jamii na taasisi hazina budi
kushirikiana ili kuokoa hali ya mazingira.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba. |
Taarifa hiyo imekuja kufuatia hotuba ya bajeti ya
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati
akizungumzia hifadhi endelevu ya mazingira bungeni mjini Dodoma.
Mh Makamba amesema kuwa kutokana na Sekta zote za
maendeleo ya mwanadamu kutegemea mazingira, hali ya mazingira imeendelea kuonesha
taswira ya kuwa jangwa hivyo jitihada zinahitajika ili kukabiliana na hali
hiyo.
Aidha, amesema kuwa zipo bidii mbali mbali zinazofanyika
na serikali katika kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa katika hali nzuri ikiwemo
sera na sheria za mazingira kuendelea kusimamiwa kikamilifu pamoja na miradi ya
usimamizi wa mazingira kwa mujibu wa sheria na sera zilizopo.
Nayo kamati ya kudumu ya bunge ya viwanda biashara
na mazingira imeishauri serikali kuendelea kusimamia sheria na sera ya mzingira
kikamilifu katika maeneo mbalimbali nchini.
SERIKALI IMESEMA KUWA BADO KUNA UWEPO WA VIASHIRIA VYA HATARI KATIKA MAZIMGIRA.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments