SERIKALI INAMPANGO MAHUSUSI KWA ZAO LA ALIETI.
Serikali imesema kuwa imeweka mkakati mkubwa wa
kuhakikisha kuwa zao la alizeti linazalishwa kwa wingi ili mafuta ya kutosha yaweze
kupatikana na kusaidia kukuza uchumi wa nchi pamoja na wakulima wa maeneo
yanaozalisha zao hilo.
Zao la Alizeti. |
Hayo yamebainishwa bungeni mjini Dodoma na waziri wa
kilimo Dk. Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mh. Matha
Mlata kwa niaba ya waziri wa Viwanda Biashara na Uwezeshaji aliyetaka kujua
kwanini ruzuku za mbegu ya zao la alizeti
hazijatolewa kwa wakulima ili kukidhi haja ya viwanda vinavyojengwa mkoani
Singida.
Dk. Charles Tizeba. |
Aidha, amesema kuwa serikali ina mkakati mahususi kwa
zao la alizeti ambapo mkakati huo mbali na mambo mengine unalenga kuongeza uzalishaji
wa zao la alizeti hapa nchini pamoja na usindikaji wa mazao yanayotokana na zao
hilo.
Usindikaji wa zao la Alizeti. |
Dkt Tizeba amesema kuwa mkakati huo umeanza ili kuhakikisha
kuwa upatikanaji wa mbegu bora za alizeti unakuwa na utoshelevu ambapo aina nne
za alizeti tofauti mpya zimekwisha kupatikana ambazo ni bora kuliko mbegu
zilizokuwa zikitumika nchini kwa muda mrefu.
Varayati za aina ya mbegu za alizeti. |
Hata hivyo amesema kuwa, awali mbegu zenye kuzalisha
mafuta mengi kwa sasa zimepatikana katika aina nne na hivyo zitaanza kusambazwa
kwa wakulima hapa nchini huku lengo lake likiwa ni kuzalisha malighafi za kutosha
kwa ajili ya viwanda vinavyojengwa nchini.
SERIKALI INAMPANGO MAHUSUSI KWA ZAO LA ALIETI.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments