RAYMOND MUSHI AWATAKA WANANCHI KUACHA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI ILI KUIMARISHA MAENDELEO MBALI MBALI KIJAMII.
Wananchi
wa kijiji cha Sangara katika kata ya Riroda wilayani Babati mkoani Manyara
wametakiwa kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji badala yake
watumie fursa ya kupatikana kwa maji kuvutia maendeleo ikiwemo
kuimarisha makazi bora, usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora.
Akitambulisha
mradi mpya wa majaribio wa maji na usafi wa mazingira katika kijiji
cha Sangara Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi amesema kuwa ni
muhimu wakatambua kuwa miradi inayojengwa na serikali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo ni miradi yao na kwamba ni lazima kuilinda,kusimamia na
kuiendeleza.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi. |
Amefafanua
kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu katika maeneo mengi duniani kunaongeza pia
matumizi makubwa ya maji jamii inatakiwa iangalie ajenda ya maji kuwa ya kudumu
ili kunusuru jamii husika na ukosefu wa maji.
Kwa
mujibu wa Bw Mushi migogoro mingi ya wakulima na wafugaji mkoani Manyara
inatokana na watu kupigania maji hivyo wananchi wa kijiji cha Sangara
wanatakiwa kushirikiana na wataalamu katika ujenzi wa miundo mbinu hiyo nakuwa
tayari kuchangia gharama za maji wakati ukifika.
Naye Mkurugenzi
Mkaazi wa shirika la Water Aid Tanzania Dr. Ibrahim Kabole amesema kuwa mradi
huo wa majaribio katika kijiji cha Sangara unatekelezwa kwa miezi 24 kuanzia
tarehe 15 Novemba 2017 hadi 31 Oktoba 2019 kwa ushirikiano wa Halmashauri ya
wilaya ya Babati, shirika la Habitat for Humanity (HFHT),UTT Micro Finance,na Water pay limited ambapo unatarajia
kuwahudumia wananchi,2700.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Sangara, Martin Masong’ ameishukuru
serikali kupitia shirika la Water Aid Tanzania kuondoa kero ya maji kwa kijiji
hicho na vijiji jirani kwani walikuwa wakitumia punda kwenda umbali wa kilomita
8 kutafuta maji.
RAYMOND MUSHI AWATAKA WANANCHI KUACHA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI ILI KUIMARISHA MAENDELEO MBALI MBALI KIJAMII.
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:
No comments