MAGAIDI 15 WAUAWA KATIKA MJI WA KIHISTORIA WA TIMBUKUTU MALI.


Serikali ya Ufaransa imesema kuwa magaidi 15 wameuawa katika mji wa Kihistoria wa Timbukutu Kaskazini mwa Mali, baada ya uvamizi katika kambi ya wanajeshi wa kulinda amani.
Image result for mji wa Kihistoria wa Timbuktu Kaskazini mwa Mali,
Mji wa Kihistori wa Timbuktu.
Uvamizi huo ulisababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA) baada ya kurushwa kwa vilipuzi katika kambi hiyo,ambapo taarifa za kijeshi nchini Ufaransa zinasema, wanajeshi wake saba walijeruhiwa.
Uvamizi huo ulifanyika katia kambi ya kikosi ha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) na kambi ya kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane.
Mashambulizi hayo yalidumu saa nne na magadi walikua wamejihami vya kutosha, kwa mujibu wa msemaji wa kikosi cha askari wa Ufaransa, Barkhane.

MAGAIDI 15 WAUAWA KATIKA MJI WA KIHISTORIA WA TIMBUKUTU MALI. MAGAIDI 15 WAUAWA KATIKA MJI WA KIHISTORIA WA TIMBUKUTU MALI. Reviewed by safina radio on April 16, 2018 Rating: 5

No comments