VIONGOZI WA KOREA KUSINI NA KASKAZINI WAKUTANA
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa
Korea Kusini Moon Jae-in wanafanya mkutano wa kilele wa kihistoria, baada ya
kupeana mikono katika eneo la mstari wa kijeshi ambao unazitenganisha nchi zao,
katika ishara yenye ujumbe mkubwa.
![]() |
KIM KUSHOTO NA MOON KULIA |
Kim alimwambia
Moon kuwa ana furaha kukutana naye, kabla ya mgeni huyo kuvuka upande wa Korea
Kusini, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kukanyaga Kusini
tangu vita vya Korea vilipomalizika miaka 65 iliyopita.
Kutokana na
mwaliko wa Kim, viongozi hao wawili walivuka na kuingia upande wa Kaskazini
huku wakiwa wameshikana mikono kabla ya kuingia katika Jumba la Amani upande wa
Kusini wa kijiji cha Panmunjom kwa ajili ya mkutano wao wa kilele ambao ni wa
tatu wa aina hiyo tangu uhasama ulipositishwa mwaka 1953.
Hata hivyo Kim amemwambia Moon kuwa mkutano huo ni
mwanzo wa historia mpya ambapo Moon alimjibu akisema anatumaini kuwa watafikia
makubaliano muhimu ili kuwapa zawadi watu wote wa Korea na watu wanaotaka
amani.
VIONGOZI WA KOREA KUSINI NA KASKAZINI WAKUTANA
Reviewed by safina radio
on
April 27, 2018
Rating:
No comments