WALIOVAMIA ENEO LA RELI WAANZA KUPEWA ELIMU


Shirika la Reli Nchni TRL limeanza kutoa elimu kwa watu waliovamia maeneo ya reli ndani ya mita thelathini kusogea mbali na maeneo hayo ili kurahisishia serikali kutekeleza miradi miwili ya reli iliyokusudiwa kwa manufaa ya taifa.

Image result for PICHA YA RELI

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw Adam Mgoyi amewataka wafugaji wote waliovamia maeneo ya reli kuondoka haraka iwezekanavyo wakati zoezi hilo la utoaji wa elimu kwa wananchi wa Kilosa linaendelea.

Kwa upande wa wafugaji waliovamia maeneo hayo yanayomilikiwa na  TRL wameomba serikali iwatafutie maeneo mbadala ili wahamie na kupisha ujenzi wa reli hiyo.

Hata hivyo, Miradi ya reli ya kisasa katika kiwango cha kimataifa na uboreshaji wa reli ya kati ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni ukiwa katika awamu mbili yaani kuanzia Dar es salaam hadi Kilosa na Kilosa hadi Isaka.
                                               





WALIOVAMIA ENEO LA RELI WAANZA KUPEWA ELIMU WALIOVAMIA ENEO LA RELI WAANZA KUPEWA ELIMU Reviewed by safina radio on April 27, 2018 Rating: 5

No comments