UPO UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA MAUTI NDANI YA NDOA.


Jamii imetakiwa kufahamu kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufanya maombi ya kuharibu roho mauti kwenye ndoa kwani roho hiyo imekuwa ikiwatesa wengi kiuchumi,kiafya na mara nyingine kusababisha ndoa kuvinjika.
Image result for UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana imeandaa maombi maalumu ya kushughulikia roho ya mauti kwenye ndoa pamoja na uchumba ili kurejesha mahusiano mazuri.

Aidha kwa mujibu wa somo hilo adui anapopata mwanya kwenye ndoa huachilia roho ya mauti kwenye maeneo mbalimbali kama vile afya, biashara,kilimo,ufugaji,lengo likiwa ni kuharibu maendeleo pamoja na mahusiano ya wanandoa.

Pia maombi hayo yatakwenda samabamba na maombi ya kurejesha mahusiano ya uchumba uliovunjika kwa kuwaombea vijana wanaotarajia kuingia kwenye ndoa ili wakaanze maisha bila kusumbuliwa na roho ya mauti inayovuruga ndoa nyingi kwa sasa.

Hata hivyo wanandoa kesho watafundishwa namna ya kuzijua dalili za roho ya mauti pamoja na kuzishughulikia ili kunusuru mahusiano na uchumi wa familia na elimu ambayo imekuwa ikisuasua kwa watoto baada ya ndoa kuvunjika.



UPO UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA MAUTI NDANI YA NDOA. UPO UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA MAUTI NDANI YA NDOA. Reviewed by safina radio on April 20, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.