RAIS MAGUFULI AAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. Dk. John
Magufuli leo amewaapisha viongozi mbali mbali aliyowateua wiki iliyopita
wakiwemo majaji 10 wa mahakama kuu ya Tanzania.
Hafla ya
kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam ambapo
viongozi walioapishwa ni pamoja na majaji 10 wa mahakama kuu, Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa
Mashtaka.
Aidha Rais Magufuli amewaasa Majaji hao kumtanguliza
Mungu mbele pamoja na Tanzania ili kuamua mashauri kwa uweledi huku akidokeza
kuwa kwa sasa Tanzania ipo katika vita vya kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Katiba na
Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa kazi ya kuhukumu si kazi ya nyepesi bali kunahitaji uaminifu pamoja na
kutenda haki katika kutoa maauzi bila upendeleo.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma amesema kuwa
mzigo wa kusikiliza mashauri umepungua kutoka mashauri 535 hadi 460 kwa
mwaka,huku wastani wa kusikiliza mashauri kwa jaji mmoja kwa mwaka ikiwa ni
mashauri 178 lakini ambapo wastani uliowekwa na mahakama kwa sasa ya kusikiliza
mashauri kwa jaji mmoja kwa mwaka ni mashauri 220.
RAIS MAGUFULI AAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI.
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments