DKT. SIMON CHACHA AWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUTOKA JUMUIYA YA WAZAZI KURUDISHA MAADILI KWA WATOTO.


Katika kuadhimisha siku ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani Duniani,Mkoani Arusha maadhimisho hayo yameadhimishwa kwa ushirikiano wa asasi mbalimbali pamoja na Halmashauri ya jiji la Arusha ambapo Mganga Mkuu wa jiji Dkt.Simon Chacha amewataka viongozi wa vyama vya siasa walioko katika jumuiya za wazazi kurudisha maadili kwa watoto.

Image result for Mganga Mkuu wa jiji la Arusha Dkt.Simon Chacha

Ameyasema hayo leo wakatika alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo yameandaliwa na kituo cha Amani Children Home ambapo amewataka viongozi wa dini mbalimbali kuhubiri malezi bora ya watoto kwa wazizi na kuhakikisha maadili mazuri yanatekelezwa.

Aidha Dkt Chacha amesema kuwa serikali itahakikisha inawajali watoto hao kwa kuwapatia malazi na tiba bora huku akiwaomba wadau wa maendeleo ya watoto kujitoa kwa wingi katika kuwasaidia watoto ambao wanakubwa na majanga mbalimbali yakiwemo ubakaji,ulawiti na unyanyasaji wa jinsia thidi yao.

Naye Afisa Ustawi wa jamii jiji la Arusha Bi Martha George amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ni kundi ambalo linatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kifungu cha 16 juu ya kupatiwa ulinzi na kupata matunzo na haki zao za msingi.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mtoto Milton Aminiel amesema kuwa zipo sababu zinazomfanya mtoto kuingia mtaani moja wapo ikiwa ni unyanyaswaji majumbani,ugomvi wa wazazi,kutelekezwa na wazazi au walezi,umaskini,vifo vya wazazi,ushawishi wa makundi rika pamoja na sababu za dini pamoja na kimila na desturi.

DKT. SIMON CHACHA AWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUTOKA JUMUIYA YA WAZAZI KURUDISHA MAADILI KWA WATOTO. DKT. SIMON CHACHA AWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUTOKA JUMUIYA YA WAZAZI KURUDISHA MAADILI KWA WATOTO. Reviewed by safina radio on April 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.