BENDERA YA SYRIA YAPEPEA KATIKA MJI WA DOUMA.


Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema bendera ya utawala wa Syria inapeperuka katika mji wa Douma ulioko katika eneo la Ghouta Mashariki, hiyo ikiashiria kuwa majeshi ya utawala wa Syria yana udhibiti kamili wa Ghouta Mashariki.
 Image result for BENDERA YA SYRIA

Mkuu wa kituo cha maridhiano cha jeshi la Urusi nchini Syria, Meja Jenerali Yury Yevtushenko amesema leo ni siku ya kihistoria nchini Syria kwani kupeperushwa kwa bendera ya utawala wa Syria ni ishara tosha ya udhibiti kamili wa mji wa Douma na Ghouta Mashariki nzima.

Serikali ya Syria yenyewe bado haijatangaza rasmi kuwa inaidhibiti Douma ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya waasi katika eneo la Gouta Mashariki, huku Wizara ya ulinzi ya ikimesema wanajeshi wake wameanza kushika doria katika mji huo.

Hata hivyo Shirika la kutetea haki za binadamu Syria limesema waasi wa kundi la Jaish al Islam wamesalimisha silaha zao nzito na kiongozi wao Issam Buwaydani ameondoka Douma.

BENDERA YA SYRIA YAPEPEA KATIKA MJI WA DOUMA. BENDERA YA SYRIA YAPEPEA KATIKA MJI WA DOUMA. Reviewed by safina radio on April 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.