wananchi wanaosumbuliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha watakiwa katika ofisi za ustawi wa jamii kupatiwa ushauri.
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee
na watoto Mh Faustine Ndugulile amewataka wananchi wanaosumbuliwa na changamoto
mbalimbali za kimaisha ikiwemo msongo wa mawazo kufika katika ofisi za maafisa
ustawi wa jamii walioko katika kila wilaya ili kupata ushauri wa kisaikolojia
ili waondokane na matatizo hayo.
MH. NDUGULILE |
Mh Ndugulile ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Mh Fatma Hassan Towfik aliyetaka
kujua serikali inawasaidiaje wananchi ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali
ya kimaisha na kuwafanya kukata tamaa ya kuishi.
Amesema kuwa wananchi wengi hapa nchini wanakabiliwa
na msongo wa mawazo unaosababishwa na sababu za kimaisha ikiwemo
umaskini,kutengwa,kunyanyapaliwa,magonjwa na upweke na kuwafanya kukata tamaa
ya kuishi,hivyo ni bora wananchi wanapoona hali kama hiyo wakafika katika ofisi
hizo ili kupata ushauri.
Aidha katika hatua nyingine naibu waziri huyo
ameitaka jamii inayokumbw a na migogoro ya kifamilia kufika katika ofisi za
ustawi wa jamii zilizopo katika kila halmashauri ili kupata ushauri wa
kusuluhisha migogoro hiyo,ambapo huduma zinapatika siku zote za kazi.
wananchi wanaosumbuliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha watakiwa katika ofisi za ustawi wa jamii kupatiwa ushauri.
Reviewed by safina radio
on
April 13, 2018
Rating:
No comments