SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA VITUO VYA AFYA KWA KUWEKA HUDUMA ZA DHARURA.
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee
na watoto Mh Faustine Ndugulile amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha
vituo vya afya kwa kuweka huduma za dharura ili kupunguza vifo vya akina mama
na watoto njiti.

Mh Ndugulile ameyasema hayo leo bungeni jijini
Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Mh Halima
Bulembo aliyetaka kujua kuwa serikali ina mpango gani wa kuboresha huduma za
watoto njiti katika hospitali na vituo mbalimbali Vya afya.
Amesema kuwa vifo vya akina mama na watoto vimekuwa
vingi hapa nchini na serikali kwa kulitambua hilo imejiwekea mkakati wa
kuhakikisha kuwa huduma za watoto njiti na watoto wote zinapatikana katika
hospitali zote,vituo vya afya na katika hospitali za wilaya.
Aidha katika hatua nyingine naibu waziri wa nchi
ofisi ya rais TAMISEMI Mh Josephat Kandege amesema kuwa serikali inaendelea
kushughulikia ombi la kuongeza muda likizo ya uzazi kwa wanawake wanaojifungua
watoto njiti kutoka muda wa miezi mitatu hadi miezi sita.
Hata hivyo bunge la bajeti linaendelea jijini Dodoma
ambapo leo waziri wa elimu sayansi tekinolojia na mafunzo ya ufundi Mh Joyce
Ndalichako amewasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.
SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA VITUO VYA AFYA KWA KUWEKA HUDUMA ZA DHARURA.
Reviewed by safina radio
on
April 30, 2018
Rating:
No comments