imebainika kuwa ili mtu afanikiwe ni lazima kujenga madhabahu kwa unachofanya.
Imebeinika kuwa kanuni moja wapo ya mtu kufanikiwa
kiroho na kimwili ni pamoja na kuijengea madhabahu kila kitu anachokifanya kwa
kumuweka Yesu Kristo moyoni mwake,kulisoma neno na kuomba, pamoja na kufanya
kazi kwa bidii.
Redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo
mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imeandaa
mafundisho pamoja na maombi kuhusu madhabahu inavyoweza kuamua mafanikio ya mtu
yawe mazuri au mabaya.
Kwa mujibu wa somo hilo baadhi ya watu katika jamii
wamekuwa wakipitia kwenye changamoto nyingi kutokana na maisha yao kushikiliwa kwenye
madhabahu ya miungu na kuwafanya kutumikia adhabu ya
magonjwa,laana,madeni,umaskini huku wengine wakidhibitiwa wasimwabudu Mungu kwa
viwango vya juu.
Aidha njia pekee ya kuweza kuondokana na nguvu ya
madhabahu ya miungu na kumtumikia Mungu kwa viwango vya juu ni wajibu wa kila
mtu kukaa mbele za Mungu kwa muda mrefu na kumshirikisha kile anachokifanya
kama vile biashara,kilimo,ufugaji,masomo,pamoja na huduma kwa ujumla.
Hata hivyo kesho katika ukumbi wa safina redio kutafanyika
maombi maalum ya kuwafungua watu dhidi ya magonjwa sugu,migogoro ya
ndoa,madeni,laana,matatizo ya ajira,pamoja na ndoto mbaya zinazowasumbua watu
kutokana na vifungo vya nguvu za kimadhabahu.
imebainika kuwa ili mtu afanikiwe ni lazima kujenga madhabahu kwa unachofanya.
Reviewed by safina radio
on
April 13, 2018
Rating:
No comments