RAIS MAGUFULI LEO AMEZINDUA BARABARA YA KONDOA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John
Magufuli leo amezindua barabara ya Kondoa Mkoani Dodoma hadi Babati Mkoani
Manyara yenye urefu wa kilomita 251 huku akiwataka wakuu wa vitengo vya ulinzi
na usalama barabarani kusimamia sheria za barabarani ili kupunguza ajali za
mara kwa mara.
RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI. |
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Rais Magufuli
ameonya tabia ya madereva kuendesha magari wakiwa wamelewa na kutokuzingatia
sheria za usalama barabarani huku akiwataka wananchi kutokuondoa alama za
barabarani ili kuepusha kutokea kwa ajili zisizo za lazima.
Aidha amesema kuwa barabara hiyo ya Kondoa-Babati ni
sehemu ya barabara ya kaskazini inayounganisha ukanada wa kusini na kaskazini
mwa bara la Afrika amabapo nchi nane zimeunganishwa na barabara hiyo ikiwemo,
Afrika Kusini, Kenya, Ethiopia, na Misri.
Kwa upande mwingine Dk. Magufuli amesema kuwa Benki
ya Maendeleo ya Afrika imeahidi zaidi ya Dola Milioni 200 kwa ajili ujenzi wa
uwanja wa ndege wa kisasa jijini Dodoma huku akiwataka waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Prf. Makame Mbarawa na Waziri wa Fedha Philip Mpango kufuatilia suala
hilo.
Hata hivyo, ujenzi wa barabara hiyo umefadhiliwa na
Shirika la Maendeleo ya Watu wa Japani JEIKA na Benki ya Maendeleo ya Afrika
ambapo rais wa benki ya maendeleo ya Afrika Bw Akinumwi Adesina amesema kuwa
barabara hiyo itakuza uchumi wa Tanzania kutokana na kurahisisha shughuliza za
kibiashara katika ukanda wa maziwa makuu.
RAIS MAGUFULI LEO AMEZINDUA BARABARA YA KONDOA
Reviewed by safina radio
on
April 27, 2018
Rating:
No comments