URUSI YASEMA KUWA BENDERA YA UTAWALA WA SYRIA IMEPEPERUSHWA KATIKA MJI WA DOUMA, GHOUTA MASHARIKI.
Wizara
ya ulinzi ya Urusi imesema bendera ya utawala wa Syria inapeperuka katika mji
wa Douma ulioko katika eneo la Ghouta Mashariki, hiyo ikiashiria kuwa majeshi
ya utawala wa Syria yana udhibiti kamili wa eneo hilo.
Mji wa Douma. |
Mkuu wa kituo cha maridhiano cha jeshi la Urusi nchini Syria, Meja Jenerali Yury Yevtushenko amesema leo ni siku ya kihistoria nchini Syria kwani kupeperushwa kwa bendera ya utawala wa Syria ni ishara tosha ya udhibiti kamili wa mji wa Douma na Ghouta Mashariki nzima.
Serikali
ya Syria yenyewe bado haijatangaza rasmi kuwa inaidhibiti Douma ambao ulikuwa
ngome ya mwisho ya waasi katika eneo la Gouta Mashariki, huku Wizara ya ulinzi
ikisema wanajeshi wake wameanza kushika doria katika mji huo.
Hata
hivyo Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria limesema waasi wa kundi
la Jaish al Islam wamesalimisha silaha zao nzito na kiongozi wao Issam
Buwaydani ameondoka mjini Douma.
URUSI YASEMA KUWA BENDERA YA UTAWALA WA SYRIA IMEPEPERUSHWA KATIKA MJI WA DOUMA, GHOUTA MASHARIKI.
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:
No comments