TFDA YAGUNDUA KUWEPO NA MBINU YA WAFANYABIASHARA KUWEKA VIPODOZI MADUKA YA KUUZIA VIFAA VYA UJENZI.
Vipodozi vilivyopigwa marufuku vyenye kugharimu
fedha zaidi ya shilingi milioni tano vimekamatwa katika baadhi ya maduka katika
Manispaa ya Tabora baada ya mamlaka husika kufanya operesheni maalumu ya
kutafuta vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya
Magharibi Dk. Edga Mahundi amesema kuwa wamegundua kuwepo na mbinu ya wafanya
biashara kuweka vipodozi vilivyopigwa marufuku kwenye maduka ya kuuzia vifaa
vya ujenzi jambo ambalo ni kosa kisheria.
Miongoni wa wauzaji waliokamatwa wakiuza vipodozi
vilivyopigwa marufuku ni pamoja na Babuu Mwacha na Jesca Baraka waliokiri
kufanya makosa na kuahidi kutokurudia tena kosa hilo.
Naye Dk. Mahundi amesema kuwa wametoa elimu na
mafunzo mbali mbali kwa wauzaji wa vipodozi ,chakula na dawa kwa lengo la kuwafanya
watambue madhara ya kuuza vipodozi vilivyopigwa marufuku huku mamlaka ikiwataka
wauzaji kufuata sheria kanuni na taratibu za uuzaji wa bidhaa zao .
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuwafichua
wauzaji wanaokiuka sheria zilizowekwa katika biashara zao ili kupatikana kwa
bidhaa na huduma zinazokidhi viwango na vigezo kwa afya za walaji.
TFDA YAGUNDUA KUWEPO NA MBINU YA WAFANYABIASHARA KUWEKA VIPODOZI MADUKA YA KUUZIA VIFAA VYA UJENZI.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:

No comments