MAHAMMADU BUHARI ATAKUWA RAIS WA KWANZA KUZURU MAREKANI TANGU DONALD TRUMP KUSHIKA HATAMU ZA MADARAKA.


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajia kuzuru Marekani Jumatatu hii ikiwa  ni ziara rasmi ya kwanza kwa rais wa nchi ya Afrika tangu Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua madaraka nchini Marekani.
Image result for Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kushoto na Rais wa Marekani Donald Trump kulia.
Ziara ya Muhammadu Buhari inakuja baada ya ile ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel nchini Marekani.
Mkutano kati ya Rais Buhari na mwenyeji wake Donald Trump utazingatia masuala ya usalama na uchumi.
Mwaliko huo ulitolewa mnamo mwezi Januari 2017, Baada ya Donald Trump kukabidhiwa madaraka ya uongozi wa nchi alimpigia simu mwenzake wa Nigeria, Muhammadu Buhari, na kumuomba azuru Marekani.
Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kutoka bara la Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House,ambapo atakapokutana na kiongozi huyo kwa mashauriano rasmi mjini Washington.
Hata hivyo Kwa mujibu wa ikulu ya White House, mazungumzo kati ya wawili hao yatajikita kuhusu vita dhidi ya ugaidi, usalama na uchumi,ambapo  Ziara ya Rais Muhammadu Buhari inakuja ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Nigeria.

MAHAMMADU BUHARI ATAKUWA RAIS WA KWANZA KUZURU MAREKANI TANGU DONALD TRUMP KUSHIKA HATAMU ZA MADARAKA. MAHAMMADU BUHARI ATAKUWA RAIS WA KWANZA KUZURU MAREKANI TANGU DONALD TRUMP KUSHIKA HATAMU ZA MADARAKA. Reviewed by safina radio on April 30, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.