IMEELEZWA KUWA MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA YATASAIDIA UKUAJI WA UCHUMI.


Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prf. Makame Mbarawa Mnyaa amesema kuwa matumizi sahihi ya vifaa vya kiteknolojia ya TEHAMA ikiwemo simu za mkononi yatachangia ukuaji wa uchumi usioharibu mazingira.

Image result for picha ya makame mbarawa mnyaa
MH.MBARAWA

Waziri Mbarawa ameyasema hayo mjini Unguja kwenye mkutano wa nane wa wiki ya kijani ambapo amesema kuwa lengo la mkutano huo nikujadiliana namna ya kutumia TEHAMA ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, amesema kuwa Tanzania inawatumiaji wa simu za mkononi takribani milioni 42 na wanatumia vifaa mbali mbali vya kielektroniki ambapo baada ya muda fulani vifaa hivyo huisha matumizi hivyo vinatakiwa kutolewa kwenye soko kwa uangalifu mkubwa bila kuharibu mazingira kwa wanaotumia.

Amesema kuwa kutokana na wataalamu wa vifaa vya kielektroniki kutoka Shirika la Mawasiliano Duniani ITU, Tanzania itajifunza utaalamu huo unaotumika Duniani kuharibu vifaa hivyo vya kielektroniki vilivyopitwa na muda wa matumizi yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Viwango vya Shirika hilo la Mawasiliano Duniani-ITU Dk. Chaesa Li amewataka wataalamu wa TEHAMA kujadili namna bora ya kuchakata bidhaa na huduma za mawasiliano zilizopitwa na wakati.

IMEELEZWA KUWA MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA YATASAIDIA UKUAJI WA UCHUMI. IMEELEZWA KUWA MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA YATASAIDIA UKUAJI WA UCHUMI. Reviewed by safina radio on April 11, 2018 Rating: 5

No comments