WIZARA YA ELIMU KUENDELEA KUTENGA BAJETI YA KUNUNUA VIFAA VISAIDIZI KWA WANAFUNZI WALEMAVU.
Waziri wa elimu sayansi tekinolojia na mafunzo ya
ufundi Mh Joyce Ndalichako amesema kuwa wizara yake itaendelea kutenga bajeti
kwa ajili ya kununua vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu.
MH. NDALICHAKO |
Mh Ndalichako ameyasema hayo leo bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge bungeni ambapo amesema kuwa serikali
inafahamu changamoto mbalimali zinazowakabili wanafunzi wenye ulemavu ikiwemo
miundombinu ya majengo na vifaa vya kujifunzia hivyo kwa mwaka huu imetenga
bajeti kwa ajili ya kupunguza changamoto hizo.
Kwa upande wake naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu anayeshughulikia walemavu Mh Stella Ikupa amesema kuwa ili kupunguza
gharama za vifaa kwa walemavu ikiwemo miguu bandia serikali imefuta kodi kwa
vifaa hivyo ambavyo vinaagizwa kutoka nje ya nchi.
Aidha amesema kuwa lengo la serikali kuondoa kodi
hizo ni ili walemavu wanaohitaji vifaa hivyo wavipate kwa gharama nafuu.
Hata hivyo bunge la bajeti linaendelea mkoani Dodoma
ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti za wizara mbalimbali kwa mwaka wa
fedha wa 2018/2019.
WIZARA YA ELIMU KUENDELEA KUTENGA BAJETI YA KUNUNUA VIFAA VISAIDIZI KWA WANAFUNZI WALEMAVU.
Reviewed by safina radio
on
April 11, 2018
Rating:
No comments