SERIKALI YASEMA HAKUNA FEDHA YEYOTE ILIYOPOTEA
Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imesema
kuwa hakuna fedha yoyote ya serikali ya shilingi trilioni 1.51iliyopotea au
kutumika kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA ASHANTU KIJAJI |
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa fedha na
mipango Mh Ashantu Kijaji bungeni mjini Dodoma wakati akitoa kauli ya serikali
bungeni kuhusiana na taarifa zinazoenezwa na baadhi ya watu kuwa kiasi cha
shilingi trilioni 1.51 ambazo ni fedha za serikali hazijulikani zilipo.
Mh Kijaji amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka wa
2012/2017 serikali kupitia wizara ya fedha na mipango ilikuwa kwenye kipindi
cha mpito cha miaka mitano ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuandaa hesabu
za serikali kwa mfumo wa viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma
hivyo kutokana na taarifa za mfumo huo inaonesha kuwa hakuna fedha yoyote ya
serikali iliyopotea.
Ameongeza kuwa kutokana na ufafanuzi huo taarifa
zinazoenezwa na baadhi ya watu kuwa kiasi hicho cha fedha matumizi yake
hayajulikani hayana msingi wala mantiki yoyote na hawaitakii mema serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Dr John Magufuli.
Hata hivyo Mh Kijaji amewataka wabunge na wananchi
kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano ipo makini na haiwezi kuruhusu kwa
namna yoyote ile upotevu wa fedha za umma na dhamira ya serikali ni kuhakikisha
kuwa mapato yanayokusanywa hapa nchini yanatumika kwa maslahi ya wananchi wote.
SERIKALI YASEMA HAKUNA FEDHA YEYOTE ILIYOPOTEA
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments