GUTERRES AELEZEA WASIWASI WAKE KWA WANACHAMA 5 WA KUDUMU WA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
ameelezea wasiwasi wake kwa wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama
kuhusu mgogoro wa Syria, akisisitiza haja ya kuiepusha hali hiyo kuzidi kiwango
cha kudhibitiwa.
BW. GUTERRES |
Kauli za Guterres zimefuatia hatua ya baraza hilo
kushindwa kukubaliana kuhusu jibu la shambulizi linalodaiwa kuwa la sumu ambalo
lilifanywa mwishoni mwa wiki katika mji wa Douma unaodhibitiwa na waasi nchini
Syria na kuzusha hasira kote duniani.
Wakati huo huo, Urusi na Iran zimemshambulia Rais wa
Marekani Donald Trump baada ya rais huyo kusema kuwa Marekani itafanya
mashambulizi ya makombora dhidi ya serikali ya Syria kama jibu la shambulizi
linalodaiwa kuwa la silaha za sumu.
Urusi imesema inalifuatilia kwa karibu jeshi la
wanamaji wa Marekani ambalo liko njiani kuelekea baharani katika ukanda wa
pwani ya magharibi mwa Syria.
Hata hivyo Afisa mmoja mwandamizi wa Iran, ambaye
pia anamuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad, amesema nchi yake itamlinda
mshirika wake dhidi ya kile alichokiita kuwa ni uchokozi wa kigeni.
GUTERRES AELEZEA WASIWASI WAKE KWA WANACHAMA 5 WA KUDUMU WA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:
No comments