SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU ATHARI ZA KIFUA KIKUU
Serikali imesema kuwa inaendelea kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu athari za ugonjwa hatari wa kifua kikuu (TB) Kwa kupitia vyombo
mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
NAIBU WAZIRI WA AFYA FAUSTINE NDUGULILE |
Hayo yemeelezwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu
waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Faustine Ndugulile
wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambile Mh Masood Abdalah aliyetaka kujua
serikali imejiwekea mikakati gani ya kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu hapa
nchini.
Amesema kuwa lengo la serikali la kutoa elimu hiyo
ni ili wananchi wajue madhara ya ugonjwa huo ili waweze kuwahi katika vituo vya
afya mapema kwa kuwa matibabu ya kifua kikuu hutolewa bure.
Aidha naibu waziri Ndugulile amefafanua kuwa ugonjwa
wa kifua kikuu huwapata hasa watoto wadogo wenye umri chini ya miaka
mitano,wazee,wafungwa na watu wenye virusi vya ukimwi,ambapo pia hushambulia
maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo mapafu,moyo,ngozi na kila kiungo cha mwili.
Mh waziri pia amewataka wabunge kushirikiana na
serikali katika kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao wanayoishi ili wajue
namna ya kukabiliana na ugonjwa huo unaoambukizwa kwa njia ya hewa na kuwahi
matibabu mapema kwani ugonjwa wa kifua kikuu unatibika.
Hata hivyo bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini
Dodoma ambapo leo waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mh Makame Mbarawa
amewasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.
SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU ATHARI ZA KIFUA KIKUU
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments