BOMU LENYE KILO 500 LA ENZI YA VITA VIKUU VYA DUNIA LAPANGWA KUTEGULIWA.
Watu wanatarajiwa kuhamishwa leo katika sehemu kubwa ya
katikati ya mji mkuu wa Ujerumani Berlin huku wataalamu wakijiandaa kutungua
bomu la enzi ya vita vikuu vya pili vya dunia lenye uzito wa kilo 500 ambalo
limegunduliwa wakati wa shughuli za ujenzi.
Usafiri unatarajiwa kusitishwa huku zaidi ya watu elfu kumi
wakiondolewa kutoka katika maeneo hayo umbali wa mita 800 kutoka mahali bomu
lilipo, kikiwemo kituo kikubwa cha treni cha Berlin.
Shirika la usafiri wa treni Ujerumani Deutsche Bahn limesema
treni hazitaruhusiwa kusimama katika kituo hicho kuanzia saa nne na usafiri wa
treni utasitishwa kabisa kuanzia saa tano na nusu hadi saa saba mchana kwa saa
za ukanda huo.
Polisi wamesema bomu litatunguliwa saa tano na nusu lakini
huenda shughuli hiyo ikacheleweshwa hadi saa sita kamili.
Safari za ndege hazitarajiwi kukatizwa, ingawa usafiri wa
umma kuelekea uwanja wa ndege utaathirika.
BOMU LENYE KILO 500 LA ENZI YA VITA VIKUU VYA DUNIA LAPANGWA KUTEGULIWA.
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments