RAIS MAGUFULI LEO AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO MAJAJI 10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. Dk. John
Magufuli leo amewaapisha viongozi mbali mbali aliyowateua wiki iliyopita
wakiwemo majaji 10 wa mahakama kuu ya Tanzania.
RAIS MAGUFULI. |
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu
jijini Dar es salaam ambapo viongozi walioapishwa ni pamoja na majaji 10 wa
mahakama kuu, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali
na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.
Aidha Rais Magufuli amewaasa Majaji hao kumtanguliza
Mungu mbele pamoja na Tanzania ili kuamua mashauri kwa weledi huku akidokeza
kuwa kwa sasa Tanzania ipo katika vita vya kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Katiba na
Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa kazi ya kuhukumu si kazi ya kuikimbilia bali kuweka uaminifu pamoja na
kutenda haki katika kutoa maauzi yao bila upendeleo.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma amesema kuwa
mzigo wa kusikiliza mashauri umepungua kutoka mashauri 535 hadi 460 kwa mwaka
huku wastani wa kusikiliza mashauri kwa jaji mmoja kwa mwaka ikiwa ni mashauri
178 lakini ambapo wastani uliowekwa na mahakama kwa sasa ya kusikiliza mashauri
kwa jaji mmoja kwa mwaka ni mashauri 220.
Kwa upande wake Kamishna wa Maadili kwa Watumishi wa
Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewaasa majaji hao wapya kuzingatia maadili na
kuwaepuka marafiki wabaya na kuepuka upendeleo katika utendaji wao kazi.
RAIS MAGUFULI LEO AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO MAJAJI 10
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments