WAPALESTINA WATATU WAUAWA KATIKA ENEO LA UKANDA WAGAZA BAADA YA KUFYATULIWA RISASI NA WANAJESHI.


Wanajeshi wa Israel wamefyatua risasi na kuwaua wapalestina watatu katika matukio mawili tofauti yaliyofanyika mpakani mwa ukanda wa Gaza na Israel jana Jumapili.
Image result for Wanajeshi wa Israel wamefyatua risasi na kuwaua wapalestina watatu
Wanajeshi wa Israel wakiwafyatulia risasi.
Jeshi la Israel limesema wanajeshi walilazimika kuwafyatulia risasi baada ya wapalestina hao kuvuka uzio na kuingia maeneo ya Israel na kuvirushia milipuko vikosi vya Israel.
Tukio la jana Jumapili ni la hivi karibuni mpakani tangu maandamano dhidi ya Israel yalipoanza tena kwenye ukanda wa Gaza mnamo Machi 30.
Hata hivyo Wapalestina kadhaa wameuawa na maelfu wengine kujeruhiwa kutokana na vurugu ambazo zimekuwa zikifanyika maeneo hayo.

WAPALESTINA WATATU WAUAWA KATIKA ENEO LA UKANDA WAGAZA BAADA YA KUFYATULIWA RISASI NA WANAJESHI. WAPALESTINA WATATU WAUAWA KATIKA ENEO LA UKANDA WAGAZA BAADA YA KUFYATULIWA RISASI NA WANAJESHI. Reviewed by safina radio on April 30, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.