WABUNGE 500 WA EU WAIIONNYA MAREKANI.
Wabunge wapatao 500 kutoka Uingereza, Ufaransa na Ujerumani
wamelionya bunge la Marekani, Congress, kuhusu kuvurugika kwa uaminifu katika
mahusiano kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani na kuendelea kwa mzozo wa
Mashariki ya Kati iwapo Marekani itajiondoa katika mkataba wa nyuklia na Iran.
Wabunge hao wamelihimiza bunge kuunga mkono mkataba huo ambao
Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuachana nao.
Utawala wa Trump umetaka mkataba huo wa nyuklia ulioafikiwa
2015 ufanyiwe marekebisho kufikia tarehe 12 Mei mwaka huu, vinginevyo Marekani
itaiwekea vikwazo Iran na kuusambaratisha mkataba huo licha ya Iran kuuheshimu.
Hata hivyo Wabunge kutoka nchi hizo tatu ambazo ni miongoni
mwa nchi zilizoridhia mkataba na Iran wameonya kuwa Marekani kuachana na
mkataba huho heunda kukafikisha mwisho hatua zilizowekwa za kuudhibiti mpango
wa nyuklia wa Iran na kusababisha chanzo cha mzozo Mashariki ya Kati.
WABUNGE 500 WA EU WAIIONNYA MAREKANI.
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments