MATUMIZI YA SILAHA ZA SUMU NCHINI SYRIA UNASTAHILI UCHUNGUZI.
Baada ya mkutano wake wa kilele nchi zote
zilizoko katika Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu isipokuwa Syria na Qatar,
zimesema uhalifu wa matumzi ya silaha za sumu na serikali ya Syria unastahili
kuchunguzwa.
Jumuiya hiyo pia imeilaani Iran kwa kutotambua
uhuru wa nchi zingine. Katika hotuba ya ufunguzi ya Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameikosoa hatua
ya wazi ya Iran ya kuingilia masuala ya nchi zingine.
Iran ni mwandamani wa rais wa Syria Bashar
al-Assad na imekuwa ikichochea vita nchini Yemen dhidi ya Saudi Arabia.
Mkutano huo wa kilele umefanyika Saudi Arabia
na umeunga mkono kushambuliwa kwa sehemu zenye silaha za Syria kulikofanywa na
Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Lakini wanachama wengine wa Jumuiya hiyo kama
Iraq na Lebanon walikuwa wamelaani mashambulizi hayo.
Licha ya
kuwa rafiki mkubwa wa Marekani Mfalme Salman pia amemshambulia Rais Donald
Trump kwa kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
MATUMIZI YA SILAHA ZA SUMU NCHINI SYRIA UNASTAHILI UCHUNGUZI.
Reviewed by safina radio
on
April 16, 2018
Rating:
No comments