TANZANIA INATAMBUA MCHANGO WA UINGEREZA KATIKA KUZUIA UJANGILI WA WANYAMAPORI.
Makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanznaia inatambua mchango wa Uingereza
katika kuzuia ujangili wa wanyama pori hapa nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu. |
Mh Suluhu ameyasema hayo wakati alipokutana na
kufanya mazungumzo na Mwanamfalme Price Williams katika jumba la kifalme
lililopo mjini London nchini Uingereza.
Amesema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali za kupambana na kuzuia majangili ingawa bado haijawa na
tekinolojia yenye uwezo ya kuona wanyama wote lakini wanaendea kuimarisha
ulinzi wa wanyama hao.
Kwa upande wake Price William amemuahidi makamu wa
rais kuisaidia Tanzania katika ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia tekinolojia
ya hali ya juu,ambapo pia amemkaribisha rais Magufuli katika mkutano wa
kuwalinda wanyama pori unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu mjini
London.
Hata hivyo Makamu wa rais yuko mjini Uingereza
kumwakilisha rais Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya
madola.
TANZANIA INATAMBUA MCHANGO WA UINGEREZA KATIKA KUZUIA UJANGILI WA WANYAMAPORI.
Reviewed by safina radio
on
April 17, 2018
Rating:
No comments