JESHI LA POLISI MKOANI MANYARA LINAENDELEA KUFANYA UCHUNGUZI KUBAINI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO.
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara limesema
kuwa linaendelea kufanya uchunguzi ili kuwabaini wananchi wanaohamasisha maandamano
yasiyo halali kwa njia ya mtandao April 26 mwaka huu hapa nchini.
KAMANDA WA POLISI MKOANI MANYARA AUGUSTINO SENGA. |
Hayo yamesemwa na kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Manyara kamishna msaidizi wa polisi Augustino Senga wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya namna jeshi hilo
lilivyojipanga kupambana na waalifu wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani mkoani
humo.
Kamanda Senga amesema kuwa katika
mkoa wa Manyara kumekuwa na taarifa za maandamano hivyo kwa sasa wanaendelea na
uchunguzi ili kuwabaini wale ambao wanaohamasisha maandamano hayo ili waweze
kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Amewataka wananchi kuelewa
kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria kwa kuwa hayana kibali hivyo
wasikubali kufuata mkumbo na kutumika vibaya na watu wasiolitakia mema Taifa la
Tanzania.
Hata hivyo amewataka
wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu ambazo hazivunji usalama,hakiwala amani
ambao utaweza kuathiri maisha ya watu na mali zao.
JESHI LA POLISI MKOANI MANYARA LINAENDELEA KUFANYA UCHUNGUZI KUBAINI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO.
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments