RAIS WA AFRIKA YA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA AMESITISHA ZIARA YAKE NCHINI UINGEREZA
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelazimika kusitisha
ziara yake nchini Uingereza anakohudhuria mkutano wa viongozi kutoka mataifa ya
Jumuiya ya Madola ili kurejea nyumbani kutokana na machafuko yanayoshuhudiwa
Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
RAIS WA AFRIKA YA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA |
Wakaazi wa mkoa huo wamekuwa wakiandamana, na kupora mali za
wafanyibiashara hasa kutoka nje ya nchi hiyo kwa madai ya kuwa wanataka ajira,
makaazi bora na kumalizwa kwa ufisadi.
Shughuli zimekwama katika mji mkuu wa mkoa wa Mahikeng, huku
maduka yakisalia kufungwa na waandamanaji kuteketeza kwa moto matairi
barabarani wakitaka pia kujiuzulu kwa viongozi wa mkoa huo.
Rais Ramaphosa anarejea nyumbani kujaribu kumaliza machafuko
hayo ambayo yameelezwa na kiongozi wa eneo hilo Supra Mahumapelo kuwa
yamechochewa kisiasa.
Hata hivyo Kuporwa kwa mali na uharibu unatokea ni pigo kwa
serikali ya rais Ramaphosa ambaye wiki hii, ametumia muda mwingi akiwa jijini
London kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini humo.
RAIS WA AFRIKA YA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA AMESITISHA ZIARA YAKE NCHINI UINGEREZA
Reviewed by safina radio
on
April 20, 2018
Rating:
No comments