TANAPA YAHAKIKISHA INAREJESHI MAWAILIANO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NDANI YA HIFADHI YA ZIWA MANYARA.
Hali ya miundombinu katika hifadhi ya ziwa manyara
iliyoharibiwa na mvua hususani daraja la Marera imerejea kufuatia jitihada
zilizofanywa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Nchini TANAPA.
![]() |
Meneja wa Mawasiliano wa TANAPA Paskali Shelutete. |
Meneja wa Mawasiliano wa TANAPA Paskali Shelutete
amesema kuwa miundombinu katika hifadhi hiyo iliharibiwa pakubwa na maji ya
mvua na kusababisha vivutio vya utalii kutokufikika kwa urahisi.
Aidha, amesema kuwa wamefanya mazungumzo na wadau wa
utalii ambao ni wageni wanaofika katika maeneo hayo ambapo wamewataka wasitishe
ratiba za safari zao za utalii kwa muda ili Mamlaka iweze kurejesha hali ya miundombinu
iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hata hivyo amewatoa wasiwasi wadau hao wa utalii
wanaopenda kuitembelea hifadhi hiyo kwa kuwa
Mamlaka ya hifadhi za taifa imeimarisha vikosi vya dharura kwa lengo la
kuhakikisha kuwa miundombinu inaendelea kupitika hasa kipindi hiki cha mvua.
TANAPA YAHAKIKISHA INAREJESHI MAWAILIANO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NDANI YA HIFADHI YA ZIWA MANYARA.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:

No comments