RAIS MAGUFULI ABADILISHA VYEO VYA MAAFISA NDANI YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA JWTZ.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli leo Aprili 12, 2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania JWTZ katika vyeo mbalimbali.
![]() |
Rais Magufuli. |
Taarifa hiyo ilisomwa na Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es
Salaam ambapo imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali
Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya
Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli TMA na kwa uteuzi
huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.
Aidha, Mhe. Dk. Magufuli amempandisha cheo
Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali huku akiwapandisha vyeo
maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1
kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.
Hali kadhalika waliopandishwa vyeo hivyo
ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga, Z.S
Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M
Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.
Wengine ni C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C
Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S Ismail, M.N Mkeremy, G.S
Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.
Vile vile, Mhe.
Rais Magufuli amempandisha cheo Luteni Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali
na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais-AIDE DE CAMP – ADC akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka
Naziad Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.
RAIS MAGUFULI ABADILISHA VYEO VYA MAAFISA NDANI YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA JWTZ.
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:

No comments