MBUNGE WA BABATI VIJIJINI MH.JITU SONI AKABIDHI MABATI 230 KATIKA KITUO CHA AFYA GALAPO.
Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini, Mkoani
Manyara Jitu Soni ametoa mabati 230
yenye thamani ya sh. Mil.5.6 kwa ajili ya upauzi wa jengo la upasuaji katika
kituo cha Afya cha Galapo wilayani Babati vijijini.
MBUNGE WA BABATI VIJIJINI MH. JITU SONI. |
Akizungumza na
wananchi wa Galapo, mbele ya wabunge 6 alioongozana nao, mbunge huyo amesema
anawashukuru wabunge hao kwa kuunga mkono juhudi zake na za wananchi wake
kiujumla kwa kuchangia jumla ya sh.mil.1.4 kwa ajili ya kukamilisha jengo hilo
la upasuaji.
Mh Soni amesema kuwa jengo hilo la upasuaji katika kituo cha afya
cha Galapo litakapokamilika litakua ni msaada mkubwa kwani litawaondolea adha wananchi ya kwenda
hospitali ya Mrara ama ya mkoa kufuata huduma hiyo.
Aidha mbunge huyo Soni
alitumia fursa hiyo pia kumshukuru mbunge wa jimbo la Kiteto Emmanuel
Papian kwa kumuunga mkono katika hatua za awali za ujenzi wa jengo hilo
kwa kuchangia sh.mil.2.8, ambapo amesema msaada huo uliweza kufanikisha kwa
kiasi kikubwa katika ujenzi wa jengo
hilo la upasuaji.
Akiongea kwa niaba ya
wabunge wa Mkoa huo, mwenyekiti wa wabunge, mbunge wa jimbo la Hanang
Dkt.Mary Nagu alimpongeza mbunge Jitu Soni kwa kuwashirikisha katika shughuli
zake za maendeleo ya Jimboni kwake, lakini kubwa lililowavutia ni uchapakazi
wake.
Kwa upande wake
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hamisi Malinga alisema kuwa kutolewa
kwa mabati hayo na fedha hizo kutapunguza mzigo mkubwa kwa wananchi wa
kuchangia na kutawezesha kukamilika kwa haraka kwa kituo hicho na
kusaidia wananchi kuondokana na kutafuta huduma mbali.
UNAENDELEA KUSIKILIZA
TAARIFA HII YA HABARI
MBUNGE WA BABATI VIJIJINI MH.JITU SONI AKABIDHI MABATI 230 KATIKA KITUO CHA AFYA GALAPO.
Reviewed by safina radio
on
April 16, 2018
Rating:
No comments