UGANDA ITAANZA KUTOA CHANJO YA KIPINDUPINDU BAADA YA VIFO VYA WATU 44 HUKU ZAIDI YA 2000 KULAZWA.


Wizara ya afya nchini Uganda itaanza kutoa chanjo ya ugonjwa wa kipindupindu ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo katika kambi za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC uliosababisha vifo vya watu 44 na wengine zaidi ya elfu 2 kulazwa tangu mwezi Februari mwaka huu.

Image result for UGANDA
Uganda.
Kaimu mkurugenzi wa huduma za afya nchini humo Charles Olaro amesema, chanjo hiyo imepangwa kuanza mwezi ujao na itatolewa katika kambi za wakimbizi za Kyangwali na Kyaka II, ambazo ziko kwenye wilaya za magharibi za Hoima na Kyegegwa.

Bw. Olaro amesema chanjo hiyo pia itatolewa katika maeneo mengine nchini Uganda ikiwemo Buliisa, Pakwach, Kasese, na Zombo.

UGANDA ITAANZA KUTOA CHANJO YA KIPINDUPINDU BAADA YA VIFO VYA WATU 44 HUKU ZAIDI YA 2000 KULAZWA. UGANDA ITAANZA KUTOA CHANJO YA KIPINDUPINDU BAADA YA VIFO VYA WATU 44 HUKU ZAIDI YA 2000 KULAZWA. Reviewed by safina radio on April 17, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.