TATIZO LA MIGOGORO SUGU YA ARDHI SASA KUTATULIWA SINGIDA.


Tatizo sugu la migogoro ya mipaka baina ya vijiji, kata na wilaya ya jirani na Halmashauri ya Itingi Mkoani Singida huenda likatatuliwa baada ya kununuliwa kwa vifaa vya kisasa vinavyogharimu mamilioni ya fedha zenye uwezo wa kubaini alama za mipaka ya zamani ili kuondoa utata.

Hayo yamebainika kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Pius Mhende na Mtaalamu wa Upimaji Ardhi Juma Rashidi kupitia vifaa hivyo vya kisasa vyenye thamani ya fedha shilingi milioni 54.

Madiwani wamekuwa na matumaini kuwa vifaa hivyo vitamaliza migogoro ya ardhi,mipaka pamoja na kupima viwanja vya makazi ya watu ili kuwezesha kutumia rasilimali hiyo kujikomboa kiuchumi.

Kabla ya kununuliwa kwa vifaa hivyo vyenye uwezo wa kupima zaidi ya viwanja 100 kwa saa ishirini na nne halmashauri ya wilaya ya Itigi ilikuwa ikodi vifaa hivyo kwa shilingi laki tatu kwa siku kwa kupima makazi ya wananchi wake kwa lengo la kumaliza migogoro ya mipaka.
                     

TATIZO LA MIGOGORO SUGU YA ARDHI SASA KUTATULIWA SINGIDA. TATIZO LA MIGOGORO SUGU YA ARDHI SASA KUTATULIWA SINGIDA. Reviewed by safina radio on April 26, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.