UINGEREZA, UFARANSA, UFARANSA NA UJERUMANI YAAHIDI KUUNGA MKONO MAKUBALIANO YA SASA YA NYUKLIA, IRAN.
Viongozi wa Uingereza , Ufaransa na Ujerumani
wameahidi kuunga mkono makubaliano ya sasa ya nyukilia yaliyofikiwa mwaka 2015
kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu duniani.

Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza viongozi wa
nchi hizo tatu wamesema makubaliano hayo ni njia nzuri inayosaidia kupunguza
kitisho cha silaha za nyukilia cha Iran.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alizungumza kwa simu na rais wa
Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mwishoni
mwa wiki na viongozi hao wakakubaliana kuwa njia pekee ilikuwa ni kuyalinda
makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 2015.
Hata hivyo rais Donald Trump wa Marekani
amekuwa akitishia kujiondoa kwenye makubaliano hayo ambapo mwezi Mei huenda
akafanya uamuzi.
UINGEREZA, UFARANSA, UFARANSA NA UJERUMANI YAAHIDI KUUNGA MKONO MAKUBALIANO YA SASA YA NYUKLIA, IRAN.
Reviewed by safina radio
on
April 30, 2018
Rating:

No comments