RAIS MAGUFULI APANDISHA HADHI MANISPAA YA DODOMA KUWA JIJI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  ametangaza  rasmi  mkoa  wa  Dodoma  kuwa  jiji  badala  ya  kuitwa  manispaa  wakati akiwa  mgeni  rasmi  katika  maadhimisho ya Sherehe  za Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini  humo.
Image result for magufuli

Mh.Magufuli  ametangaza Dodoma  kuwa  jiji ili kuinua  hadhi ya  makao makuu  ya nchi  na  kuongeza  idadi  ya  majiji nchini sanjari  na kumtangaza aliyekuwa mkurugenzi wa  mji wa Dodoma  kuanzia  sasa  kuwa ataitwa  mkurugenzi  wa  jiji.

Aidha  mheshimiwa  Rais ameagiza  taasisi zinazohusika na  mipango ya  majiji  kuandaa  mipango  yote  ya  kiserikali  kuhusu  Dodoma  sasa  yawe  yanafanyika kwa  kuzingatia  kuwa  Dodoma ni  jiji.

Vile vile  Rais Magufuli  amesema serikali  ya  jamhuri  ya  muungano  wa Tanzania italinda muungano kwa  namna  yeyote  na  kamwe  haitamwonea aibu,huruma  wala haya mtu  yeyote atakaye jaribu  kuvunja  amani na  muungano  wa  jamhuri  ya  muungano  wa Tanzania.

Hata  hivyo  mheshimiwa  Rais  pamoja  na  kutangaza  Dodoma  kuwa  jiji  amesema  kuwa  mwaka  huu  atahamia  Dodoma .

RAIS MAGUFULI APANDISHA HADHI MANISPAA YA DODOMA KUWA JIJI. RAIS MAGUFULI APANDISHA HADHI MANISPAA YA DODOMA KUWA JIJI. Reviewed by safina radio on April 26, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.