ZOEZI LA UTOAJI WA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI WAANZA ARUSHA.
Kaimu mkuu wilaya ya Arumeru ambaye pia ni mkuu wa
wilaya ya Monduli Bw. Idd Kimanta amesema kuwa serikali itachukua hatua kali za
kisheria kwa mtu yeyote Yule
atakayejaribu kukwamisha zoezi la utoaji chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.
Bw Kimanta ametoa kauli hiyo wakati akizindua zoezi
la utoaji chanjo hiyo katika hospitali ya wilaya Tengeru ambapo amewataka viongozi
wote wanaohusika wakiwemo wakuu wa shule,watendaji wa kata, maafisa elimu
pamoja na wenye viti wa maeneo yote kusimamia vizuri zoezi hilo bila kuingiza
kikwazo chochote.
Amesema kuwa serikali imekusudia
kutoa chanjo hiyo ili kusaidia kinga ya maambukizi ya
saratani ya mlango wa kizazi kwa kizazi kijacho hasa kwa wasichana wadogo hivyo
serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayekwamisha zoezi hilo.
Kwa upande wa mganga mkuu wa wilaya hiyo Dr Cosmas
Kilasara amesema kuwa jumla ya wanawake
5892 wamefanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo ambapo 319 waligundulika kuwa na
dalili za awali huku 19 kati yao wakipatiwa rufaa ya kwenda hospitali ya Ocean
road baada ya kugundulika kuwa saratani hiyo imesambaa zaidi mwilini.
ZOEZI LA UTOAJI WA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI WAANZA ARUSHA.
Reviewed by safina radio
on
April 25, 2018
Rating:
No comments