SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA HUSUSANI KUONGEZA WATOA HUDUMA ZA AFYA.
Wakazi wa Kijiji cha Muguhesi Wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
kuongezwa kwa watoa huduma kwenye kituo cha afya kilichopo kijijini hapo.
![]() |
Watoa huduma. |
Ombi hilo wamelitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kijijini hapo uliokutanisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tunduru na
Viongozi wa Kijiji.
Wakizungumza katika Mkutano wa Hadhara wakazi wa
Kijiji hicho wamesema kuwa kituo hicho cha afya kina wauguzi wawili tu hali inayosababisha
msongamano kutokana na wingi wa wagonjwa.
Naye Mkuu wa kituo hicho cha afya Esata Milanzi
amesema kuwa kituo hicho kinahudumia zaidi ya vitongoji sita na kusababisha kuelemewa
na wingi wa wagonjwa hasa wakinamama wajawazito.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Kohomera
amekiri kuwepo kwa wingi wa wagonjwa katika kituo hicho hivyo ameahidi
kulifanyia kazi ombi hilo huku kituo hicho kikiwa kinawahudumia zaidi ya
wagonjwa 46 katika vitongoji zaidi ya sita.
SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA HUSUSANI KUONGEZA WATOA HUDUMA ZA AFYA.
Reviewed by safina radio
on
April 30, 2018
Rating:

No comments