KIGOMA SASA KUUNGANISHWA KATIKA GRIDI YA TAIFA KUTOKA KIGOMA.


Waziri wa Nishati Mh Dkt.Merdad Kalimani amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya Kaliuwa na Urambo mkoani Tabora na kuunganisha mkoa wa Kigoma kwenye Gridi ya Taifa Serikali imetenga bilioni 10 kwa ajili ya kujenga vituo viwili vya kupooza na kuongeza umeme katika mikoa hiyo.

Image result for Waziri wa Nishati Mh Dkt.Medadi Kalimani
Dk. Merdad Kalimani.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika wilaya za Kaliuwa na Urambo waziri Kalimani amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo hautachukuwa muda kuanza ambapo kituo kimoja kitajengwa mpakani mwa Kaliuwa na Urambo na kingine kitajengwa mpakani mwa wilaya ya Kaliuwa na Uvinza.

Akiwa katika kijiji cha Jionee Mwenyewe Wilayani Urambo, Waziri Kalimani amezindua mradi wa usambazaji wa umeme vijijni kwa kupitia Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijni REA awamu ya tatu.

KIGOMA SASA KUUNGANISHWA KATIKA GRIDI YA TAIFA KUTOKA KIGOMA. KIGOMA SASA KUUNGANISHWA KATIKA GRIDI YA TAIFA KUTOKA KIGOMA. Reviewed by safina radio on April 18, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.