WAISRAEL LEO WAMEKAA KIMYA KWA MUDA KUKUMBUKA MAANGAMIZI YA WAYAHUDI MILIONI 6.
Wananchi
wa Israel leo wamekaa kimya kwa muda kukumbuka maangamizi ya Wayahudi milioni
sita katika mauaji ya halaiki ya Holocaust yaliyofanywa na wanazi miaka
iliyopita.
![]() |
Mauaji ya halaiki ya Holocaust. |
Ving’ora
vimelia kwa dakika mbili kote nchini Israel kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji
hayo, ambapo Shughuli za kawaida nchini humo zimesimama kwa muda kwa ajili ya
kumbukumbu hiyo.
Wakati
huohuo Maelfu ya Wayahudi wanatarajiwa kuandamana leo kutoka iliyokuwa kambi ya
mateso ya Eshwets hadi Beknau nchini Poland kama sehemu ya makumbusho hayo.
Rais wa Israel Reuven Rivlin atawaongoza
takriban watu elfu kumi na mbili watakaoshiriki katika maandamano hayo ya
Poland.
Wakati
hayo yakijiri, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameionya Iran
kutoijaribu nchi yake, na kuilinganisha na utawala wa wanazi, akiongeza kuwa
onyo lake siyo maneno matupu.
WAISRAEL LEO WAMEKAA KIMYA KWA MUDA KUKUMBUKA MAANGAMIZI YA WAYAHUDI MILIONI 6.
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:
No comments