MKOA WA KIGOMA UNAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI WA AFYA ZAIDI YA ELFU TATU


Imeelezwa kuwa mkoa wa Kigoma una upungufu wa watumishi wa afya wapatao elfu tatu mia tatu arobaini na nne ikiwa ni upungu wa asilimia 66 ya watumishi hao.

Image result for PICHA YA JOSEPHAT KANDEGE NAIBU WAZIRI TAMISEMI
MH. KANDEGE NAIBU WAZIRI TAMISEMI

Hayo yameelezwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Josephat Kandege wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu mkoa wa Kigoma Mh Josephine Gezebuke aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka watumishi wa afya katika hospitali za wilaya na vituo vya afya katika mkoa huo.

Amesema kuwa kwa mujibu wa Ikama mpya ya serikali ya mwaka wa 2014  mkoa wa Kigoma unataikiwa kuwa na watumishi wa afya elfu tano na saba lakini walioko sasa ni elfu moja mia sita sitini na tatu pekee sawa na asilimia 33.2

Ameongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo serikali ilijiwekea mipango mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 mkoa wa Kigoma ulipatiwa watumishi wa afya 95 wakiwemo madaktari 5,matabibu 24 wauguzi 33 wafamasia 17 na wataalamu wa maabara 16.

Aidha naibu waziri Kandege amesema katika mwaka wa fedha wa 2018/2019  serikali itaendelea kupunguza tatizo hilo kwa kuajiri  watumishi wa afya wenye kada mbalimbali kwa kadri fedha zitakavyopatikana.

Hata hivyo mkutano wa 11 wa bunge unaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti za wizara mbalimbali katika mwaka wa fedha wa 2018/2019.

MKOA WA KIGOMA UNAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI WA AFYA ZAIDI YA ELFU TATU MKOA WA KIGOMA UNAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI WA AFYA ZAIDI YA ELFU TATU Reviewed by safina radio on April 12, 2018 Rating: 5

No comments