AMISOM YAPOGEZA ASKARI WA UGANDA.
Tume
ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM jana imewapongeza askari wa Uganda
kutokana na juhudi zao za kuhakikisha kuwa usalama na utulivu unakuwepo nchini
Somalia na kukamilisha majukumu yao kwa bidii.
Pongezi
hizo zimetolewa na Naibu Kamanda wa Vikosi vya AMISOM Bw. Salvator Harushimana ambapo
amesema kuwa katika kipindi cha majukumu yao ya kulinda amani , askari wa
Uganda wamefanya kazi kwa kujitolea na kwa njia za kitaaluma.
Hata
hivyo, Bw. Harushimana amesema kuwa askari hao si kama tu wanawakilisha Uganda,
bali pia ni fahari ya bara la Afrika.
AMISOM YAPOGEZA ASKARI WA UGANDA.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments