WANACHAMA 30 WA AL-SHABABU WAMEUAWA.
Wanachama 30 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab
lenye mfungamano na mtandao wa al-Qaeda wameuawa katika operesheni kali
iliyotekelezwa na Jeshi la Taifa la Somalia katika eneo la Hiran jana Jumanne.

Msemaji wa jeshi katika eneo hilo Mohammad Nur Agajof, amesema
kuwa magaidi hao wameuawa katika operesheni ya jana Jumanne katika miji ya
Beledwein, Mahas na Mataban katika eneo la Hiran, katikati ya nchi hiyo ya
Pembe ya Afrika.
Amesema mbali na kuangamiza makumi ya wanamgambo hao, askari wa
Somalia wameteka Kamandi Kuu ya magaidi hao katika eneo hilo, sanjari na
kupata silaha za kijeshi zilizokuwa mikononi mwa wapiganaji hao wa Kitakfiri.
Haya yanajiri siku chache baada ya wanachama wa al-Shabaab
kutekeleza shambulizi la kigaidi na kuwaua watu watano katika uwanja wa mpira
wa miguu katika mji wa Pwani wa Barawa kusini mwa Somalia.
Kundi hilo
limeanzisha hujuma zake nchini Somalia mnamo mwaka 2007 kwa lengo la kuiondoa
madarakani serikali ya nchi hiyo kwa kile wanachokiita kuwa ni serikali ya
kikafiri.
WANACHAMA 30 WA AL-SHABABU WAMEUAWA.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:

No comments