TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINE ULIMWENGUNI KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi yanayofanyika leo duniani kote.
Hapa nchini maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika uwanja wa Samora mkoani Iringa,ambapo wafanyakazi waliandamana wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohusiana na sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi.
Image result for PICHA YA MAGUFULI


Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Ofisi ya Waziri MKuu Sera Bunge Kazi na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama amesema kuwa ushirikiano baina ya Vyama vya wafanyakazi pamoja na serikali ni lazima katika kuleta mabadiliko na kuendeleza maisha ya wafanyakazi.
Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amesema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukiunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kukuza uchumi wake kwa njia ya viwanda.
Katika maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri mkuu Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa,Spika wa bunge Job Ndugai,mawaziri na viongozi wengine wa kiasiasa na wa dini.
Hata hivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu ni kuunganishwa kwa mifuko ya Hifadhi ya jamii kulenge kuboreshwa kwa mafao ya wafanyakazi.


TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINE ULIMWENGUNI KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINE ULIMWENGUNI KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI Reviewed by safina radio on May 01, 2018 Rating: 5

No comments