SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAHAKAMA NCHINI.
MH.MAVUNDE |
Hayo yameelezwa na
naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Mh Antony Mavunde wakati akijibu
maswali ya wabunge bungeni jijini Dodoma waliotaka kujua serikali ina mpango
gani wa kujenga mahakama za mwanzo hapa nchini ili kusogeza huduma za
kimahakama karibu na wananchi.
Mh Mavunde amesema
kuwa kwa sasa kuna upungufu wa mahakama za mwanzo elfu tatu mia tatu na nne
hapa nchini na kutokana na upungufu huo serikali imepanga kujenga mahakama hizo
na kukarabati zingine kadri bajeti itakavyoruhusu.
Hata hivyo bunge la
bajeti linaendelea jijini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya
wizara ya viwanda na biashara kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 .
SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAHAKAMA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
May 11, 2018
Rating:
No comments