ZAIDI YA WALIMU 10,000 WAPO KATIKA MPANGO WA KUAJIRIWA NA SERIKALI ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA ELIMU NCHINI.
Ili kupunguza upungufu wa waalimu wa shule za msingi
hapa nchini serikali imesema kuwa ina mapango wa kuwaajiri waalimu zaidi ya
elfu kumi ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
![]() |
Hayo yameelezwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya
rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM Mh Joseph Kakunda wakati
akijibu maswali ya nyongeza leo bungeni jijini Dodoma,ambapo wabunge walitaka
kujua ni lini serikali itaondoa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya
elimu ikiwemo upungufu wa waalimu.
Amesema kuwa kwa sasa kinachofanyika ni baraza la
mitihani hapa nchini NECTA kukagua na
kuchambua vyeti vya waalimu walioomba nafasi hizo na watakaochaguliwa watasambazwa
katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha katika hatua nyingine Mh Kakunda amesema kuwa
serikali pia imetenga kiasi cha shilingi milioni mia tano kwa ajili ya kujenga
vyoo na nyumba za waalimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni
kuondoa changamoto zinazowakabili waalimu pamoja na wanafunzi.
Bunge la bajeti linaendelea mjini Dodoma ambapo
wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya wizara ya elimu,sayansi tekinolojia na
mafunzo ya ufundi kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyowasilishwa hapo juzi na waziri wa wizara
hiyo Mh Joyce Ndalichako.
ZAIDI YA WALIMU 10,000 WAPO KATIKA MPANGO WA KUAJIRIWA NA SERIKALI ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA ELIMU NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
May 02, 2018
Rating:

No comments