NCHI MBALIMBALI ZATAKIWA KUJENGA MFUMO BORA WA BIASHARA
Mwenyekiti
wa Shirika la Fedha Duniani IMF, Bi Christine Lagarde amesema nchi mbalimbali
zinatakiwa kujenga mfumo bora wa biashara ya kimataifa ili kukabiliana na
changamoto za mageuzi ya kidijitali katika sekta ya biashara.
BI LAGARDE |
Bi Lagarde
pia amesema, ubora wa uchumi wa dunia unategemea mzunguko mzuri wa biashara, na
kusema kuwa katika siku za karibuni, ongezeko la biashara limesukuma mbele
maendeleo ya uchumi wa dunia lakini, mfumo wa kujilinda kibashara unaoendelea
kujitokeza umezuia mwelekeo huu mzuri.
Mwnyekiti
huyo,amesema hivi sasa biashara bora inategemea biashara zaidi ya huduma,
ongezeko la kiwango cha uzalishaji na ushirikishi mzuri zaidi.
Ametoa wito kwa nchi
mbalimbali kupinga mfumo wa kujilinda kibiashara, na kuondoa vitendo
visivyokuwa na usawa vya biashara ili kujenga mazingira ya kibiashara yenye
usawa
NCHI MBALIMBALI ZATAKIWA KUJENGA MFUMO BORA WA BIASHARA
Reviewed by safina radio
on
May 15, 2018
Rating:
No comments